Sunday, April 30, 2017

MBEYA CITY YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KAMPUNI YA SPORTS MASTER


Katibu wa Mbeya City Emanuel Kimbe (kushoto)akipokea Vifaa kutoka kwa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Sports master Mr Fadhili Nsemwa.

Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City Mussa Mapunda (wapili kushoto) akipokea Mkataba kutoka kwa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Sports master Mr Fadhili Nsemwa mara baada ya kusaini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City Mussa Mapunda

Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Sports master Mr Fadhili Nsemwa akionyesha mfano wa Kiatu ambacho kitatumika ma wachezaji wa Mbeya City.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Katibu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe

wakiweka saini Mkataba chini ya Mwana Sheria wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.



Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Sports master Mr Fadhili Nsemwa akionyesha mfano wa Jezi ambazo zimetengenezwa na Kampuni ya Sports Master .(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)


Picha ya Pamoja Viongozi wa Mbeya City na wajumbe wa Bodi ya timu.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)



Kampuni ya sports Master imesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya mbeya city kwa ajili ya kutengeneza,kusambaza na kuuza bidhaa zinazotokana na klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.
Akiongea wakati wa zoezi hilo la utiaji saini mkuu wa biashara wa kampuni ya Sports Master Fadhili Nsemwa amesema kuwa wamejipanga katika kupambana na maharamia ambao awali walikuwa wakitumia vibaya bidhaa klabu hiyo.
                                                                                  
Kwa upande wa uongozi wa Mbeya City katibu mkuu wake Emmanuel Kimbe ameeleza kuwa wanaishukuru kampuni ya Sports Master kwa kuingia nao mkataba wa miaka miwili wa kusimamia bidhaa zao ambazo awali zilikuwa zikiuzwa kinyume cha taratibu na kunufaisha walanguzi

0 Responses to “MBEYA CITY YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KAMPUNI YA SPORTS MASTER”

Post a Comment

More to Read