Thursday, April 20, 2017

TUNISIA YARIDHIA TAMKO KURUHUSU WATU BINAFSI KUPELEKA KESI ZAO MOJA KWA MOJA KWENYE MAHAKAMA YA AFRIKA IILIYO JIJINI ARUSHA


Tunisia imesema Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) ni lazima itangazwe kwa nguvu zote ili kuwawezesha wananchi barani Afrika kufahamu uwepo wake,malengo ya kuanzishwa kwake pamoja na shughuli zake.
Akipokea ujumbe wa Mahakama hiyo katika Ikulu ya Tunisia,Rais wa Nchi Hiyo ,Mh.Beji Caid Essebsi alipongeza uanzishwaji wa Mahakama hiyo na kuongeza  kuwa inahakikisha ulinzi wa Haki za Binadamu Barani Afrika.    
 “Kwa njia hii,Haki za Binadamu Barani Afrika zitalindwa na kuhakikisha maendeleo endelevu ya demokrasia kwa wananchi” Aliuambia ujumbe huo uliohusisha majaji watatu akiwemo Rais wa AfCHPR,Jaji Sylvain Ore’.
Kwa upande wake Rais wa AfCHPR, Jaji Ore’ aliishukuru serikali ya Tunisia kwa kukubali kuupokea ujumbe wake na kukutana na Viongozi na Maafisa mbalimbali wa nchi hiyo na pia kuendesha semina kwa wadau mbalimbali nchini humo kwa lengo la kuitangaza Mahakama.
Wakati wa ziara hiyo,Tunisia ilitia saini tamko la kuruhusu watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s) katika nchi hiyo kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Mahakama hiyo yenye Makao yake makuu Jijini Arusha.
Hatua hiyo ya Tunisia ambayo ni utekelezaji wa kifungu cha 34(6),Inalifanya Taifa hilo kuwa Nchi ya nane Barani Afrika kukubali makundi hayo kupeleka kesi katika Mamlaka za Mahakama hiyo.
 Rais wa Tunisia Mh.Beji Caid Essebsi akimlaki Rais wa AfCHPR Jaji Sylvain Ore katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Tunis
Rais wa AfCHPR Jaji Sylvain Ore akionesha kwa wanahabari tamko la kuruhusu watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s) katika nchi hiyo kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Mahakama hiyo yenye Makao yake makuu Jijini Arusha.

0 Responses to “TUNISIA YARIDHIA TAMKO KURUHUSU WATU BINAFSI KUPELEKA KESI ZAO MOJA KWA MOJA KWENYE MAHAKAMA YA AFRIKA IILIYO JIJINI ARUSHA”

Post a Comment

More to Read