Thursday, April 20, 2017
TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) YAPIMA MOYO WA MTOTO ALIYE TUMBONI MWA MAMA YAKE
Do you like this story?
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Naiz amesema kuna faida lukuki iwapo mjamzito ataamua kufanya kipimo maalumu.
"Tunatumia Ultra sound kama kawaida kufanya kipimo hiki, lakini inakuwa
ina tofauti kidogo... hatutumii mionzi yoyote, hivyo hakuna madhara
anayoweza kuyapata mama au mtoto wake aliye tumboni," amesema.
TAASISI
ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara nyingine tena
imefanya upimaji wa moyo wa mtoto aliye tumboni mwa mama yake,
kuchunguza magonjwa mbalimbali ya moyo.
Upimaji huo umefanywa katika taasisi hiyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Watoto wa JKCI, Naiz Majani.
Ametaja
faida hizo kuwa ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa na
magonjwa ya moyo, na kuwaondoa kwenye masumbufu wanayoweza kuyapata
kutokana na kuchelewa kupata matibabu.
"Kwa mara ya kwanza tuliwafanyia kipimo hicho wajawazito 25 mwishoni
mwa mwaka jana ambapo watano kati yao mimba zao zilikutwa na matatizo.
Dk. Naiz akionesha jinsi wanavyofanya upimaji kuchunguza magonjwa ya moyo wa mtoto aliyeko tumboni.
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi (pichani) akielezea dhumuni la kuanzisha huduma hiyo ili kugundua matatizo mapema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) YAPIMA MOYO WA MTOTO ALIYE TUMBONI MWA MAMA YAKE”
Post a Comment