Thursday, April 20, 2017

Yatakayojiri sherehe za Miaka 53 ya Muungano


Kwa mara ya kwanza wakazi wa Mji wa Dodoma wanatarajia kushuhudia mubashara sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri.
MAKTABA: Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano
Sherehe hizo kufanyika Dodoma mwaka huu ni zimeambatana na serikali kuhamishia makao makuu yake mjini humo, na pia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama imesema kuwa sherehe hizo zitapambwa na maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na maadui hasa kulinda amani ya nchi kutoka kikosi maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wanachi Tanzania (JWTZ).
Aidha, Mhe. Mhagama amesema mambo mengine yatakayofanyika siku hiyo ni pamoja na gwaride la uzalendo la wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma,  burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi Maturumbeta.

“Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka  53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar inasema "MIAKA 53 YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUUIMARISHA, TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII" alifafanua Jenista Mhagama.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo
“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi  uwanja wa  Jamhuri siku hiyo ya Jumatano  tarehe  26 Aprili  2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,” alisema  Mhagama.

0 Responses to “Yatakayojiri sherehe za Miaka 53 ya Muungano”

Post a Comment

More to Read