Thursday, April 20, 2017

Mchezaji ajinyonga gerezani


Mchezaji wa zamani American Footballl, NFL Aaron Hernandez, aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha na siku chache zilizopita alijaribu kutaka kujiua mara mbili, amekutwa amekufa kwenye chumba cha gereza baada ya kujinyonga mapema hii leo.
Aaron Hernandez
Polisi mjini Massachusetts, imesema Hernandez alikutwa na walinzi wa Gereza la Souza-Baranowski Correctional Center, akiwa amekufa chumbani, majira ya saa 4 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka aliyofunga kwenye dirisha la chumba hicho.
Hernandez mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa zamani wa New England Patriots,alikuwa anatumikia kifungo cha maisha tangu 2015, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mtu mmoja aliyekuwa na mahusiano na dada wa mke wake, mwaka 2013.
Akiwa bado anatumikIa kifungo hicho, Ijumaa ya wiki iliyopita, Hernandez alihukumiwa tena kifungo cha miaka 5, kwa kupatikana na kesi ya mauaji ya watu wawili kwenye klabu ya usiku, mjini Boston, 2012


0 Responses to “Mchezaji ajinyonga gerezani”

Post a Comment

More to Read