Thursday, April 20, 2017
Taarifa ya ajali ya treni na daladala ya kutoka Gongo la Mboto Alfajri leo
Do you like this story?
Mtu
mmoja amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya basi la abiria/daladala
(T 435 DGG) kutoka Gongo la Mboto kwenda Mnazi Mmoja kuigonga treni ya
Pugu leo Aprili 19, 2017 saa 11 alfajiri katika makutano ya reli na
barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.
Majeruhi
wa ajali ni 23 , wanane wapo hospitali ya Amana na waliobakia 15 wapo
Hospitali ya Taifa Muhimbili MOI watatu kati yao ni mahututi. Taarifa
zaidi itatolewa kuhusu ajali hiyo.
Hata hivyo treni ya Pugu inaendelea na huduma zake kwa kufuata ratiba.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Focus Sahani,
Dar es Salaam,
Aprili 19, 2017.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)