Sunday, March 16, 2014

MAAFA JIJINI MBEYA: KAYA NANE HAZINA MAHALI PA KUISHI KATA YA ITEZI MARA BAADA YA KUEZULIWA NA UPEPO MKALI ULIOAMBATANA NA MVUA KUBWA.






Mmoja wa wahanga akiwa nje ya nyumba yake Ndugu Gaby Abson mwenye familia ya watoto wanne akiwa hajui nini cha kufanya.



Diwani Kata ya Itezi Ndugu Franky Mahemba


Jumla ya nyumba tisa   zimeezuliwa paa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo  mkali kunyesha  Jijini Mbeya.



Mvua hiyo ilianza kunyesha Machi 15 mwaka huu  majira ya saa kumi za jioni hivyo kuleta mahafa hayo katika kijiji cha Mwasote kilichopo  Kata ya Uyole ndani ya Jiji la Mbeya.



Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwasote Magharibi Ndugu  Peter Lingo amebainisha kuwa  mvua hiyo imeezua nyumba 9 na kusababisha baadhi  ya kaya kukosa mahali pa kuishi.



Aidha, amesema, tayari ameshamtahalifu Diwani wa Kata hiyo na kwamba  serikali ya kijiji imetembelea eneo husika na  kujionea hali halisi ya  wananchi waliokumbwa na  maafa hayo wakiwa wamejihifadhi kwa ndugu na jamaa zao.



Amesema, tathimini ya hasara na idadi halisi ya kaya zilizozulika na mvua hiyo bado hazijapatikana hadi pale uongozi toka Halmashauri ya jiji utakapo fika katika eneo hilo .



Hata hivyo amezitaka mamlaka husika kuliangalia suala hilo kwa uharaka zaidi ili kuokoa zaidi maafa mengine hasa kutokana na mvua hizo kuendelea kunyesha.

0 Responses to “MAAFA JIJINI MBEYA: KAYA NANE HAZINA MAHALI PA KUISHI KATA YA ITEZI MARA BAADA YA KUEZULIWA NA UPEPO MKALI ULIOAMBATANA NA MVUA KUBWA.”

Post a Comment

More to Read