Monday, March 17, 2014
TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE MAALUM KWA VYOMBO VYA HABARI
Do you like this story?
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM
TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014
Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum
inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge
Maalum utaendelea mjini Dodoma Leo kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00
asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.
Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa
kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za
Bunge Maalum kesho saa 2:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba
kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00
asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi
wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa
3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuriya
Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi
kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00 jioni
Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia
Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum
Atakaye ipata taarifa hii amjulishe
mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE MAALUM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE MAALUM KWA VYOMBO VYA HABARI”
Post a Comment