Friday, May 19, 2017
Mafuta ya Simba yamtupa Jela miaka 20
Do you like this story?
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Said Rajabu Said (36), kifungo cha
miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na mafuta ya
Simba.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri,
baada ya kumaliza ushahidi kutoka kwa mashahidi wa upande wa mashtaka
na washtakiwa kujitetea.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo kinyume na kifungu 86(1)(2)(c)(ii) ya sheria ya wanyama pori namba 5 ya 2009.
Akisoma
hukumu Hiyo Hakimu Mashauri amesema kuwa upande wa mashtaka
wamethibitisha bila kuacha shaka kuwa mshtakiwa Said ametenda kosa hilo.
Kabla
hajamsomea mshtakiwa adhabu yake, Mashauri aliuliza upande wa mashtaka
kama walikuwa na lolote la kusema ambapo wakili wa Serikali, Adolf Mkini
aliomba mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa
watu wengine wenye tabia na nia ya kutenda makosa kama hayo.
“Mheshimiwa
hakimu, sina kumbukumbu za makosa ya nyuma kwa mshtakiwa, ila naomba
mahakama yako tukufu itoe adhabu Kali kwa mshtakiwa na kwa wengine
kwenye nia ya kuharibu maliasili za nchi”, amesema Mkini.
Kwa
upande wa mshtakiwa Said katika utetezi wake ameiomba mahakama imuachie
huru kwa sababu ana watoto watano na familia inayomtegemea na yeye ndio
kila kitu kwenye familia hiyo.
”
Nimezingatia yote yaliyosemwa na upande wa mashtaka na utetezi wa
shahidi, nchi hii ina sheria zake za kulinda maliasili hivyo, Mahakama
inakuhukumu kwenda jela miaka ishirini ile iwe fundisho kwako na kwa
wengine wenye tabia kama yako”.
Mshtakiwa
anadaiwa kuwa, Februari 8,2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mafuta ya
Simba yenye thamani ya Sh 10,711,400 bila ya kuwa na kibali cha
Mkurugenzi wa wanyama pori.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)