Friday, May 5, 2017
Vitendo vya Rushwa, CCM Makete jino kwa Jino na Wanachama Leo
Do you like this story?
Wananchi wilayani Makete mkoa wa njombe wametakiwa kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume cha sheria.
Akizungumza katika mkutano na viongozi wa chama cha mapinduzi wa kata ya tandala katibu mkuu wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Lengae Godsoni Akyoo amesema vitendo vya rushwa havina budi kukemewa kwa nguvu zote.
Bw.Akyoo ameongeza kuwa kuelekea katika uchaguzi wa ndani ya chama hicho vitendo vya rushwa hivitafumbiwa macho ili kuweza kupata viongozi stahiki.
Alexanda Mbilinyi ni mmoja ya wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo naye anakiri kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika jamii na hasa nyakati za uchaguzi.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete BW. FRANSIS CHAULA amesema ili kuimarisha demokrasia mambo yote ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho yanatakiwa kufanyika kwa uwazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Vitendo vya Rushwa, CCM Makete jino kwa Jino na Wanachama Leo”
Post a Comment