Friday, May 5, 2017
Bibi auawa Kwa Risasi na mjukuu wake, Kisa Mashamba
Do you like this story?
Mkazi wa Kijiji cha Ilonga kata ya Mambwekoswe mkoani Rukwa, Sikiliel Nampunje (55) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mjukuu wake kutokana na migogoro ya mashamba.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio amesema tayari mtu huyo amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Taarifa zilizopatikana leo zinaeleza kwamba tukio limetokea juzi ambapo kijana alimuua bibi yake huyo kutokana na kwenda kwenye uongozi wa kata hiyo kudai haki yake kufuatia koporwa mashamba na ndugu zake.
Imeelezwa kuwa baada ya kijana huyo kusikia bibi yake amekwenda ofisi ya kata kudai haki yake ndipo alipomvizia njiani na kumpiga risasi.
Mume wa marehemu aitwaye Abbas Kapunda alisema mkewe alikumbwa na mkasa huo wakati akitoka kwenye shughuli zake za kilimo shambani na alikuwa akirejea nyumbani.
Amesema baada ya kusikia kelele za kuomba msaada waliamua kuelekea eneo la tukio na kumkuta mkewe akiwa anatokwa na damu eneo la kifuani ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kisha kumkimbiza katika zahanati ya kijiji ambako alifariki wakati akipatiwa matibabu.
Amesema chanzo cha kifo hicho ni mgogoro wa mashamba ambayo yalikuwa yakigombaniwa na wanafamilia hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Bibi auawa Kwa Risasi na mjukuu wake, Kisa Mashamba”
Post a Comment