Friday, May 5, 2017

Mimi ni shabiki wa Arsenal japo haifanyi vizuri – Prof. Lipumba


Ukiacha masuala ya kisiasa na ukamuuliza swali Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) taifa, Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni shabiki wa Klabu gani ya mpira wa miguu Duniani, bila kupapasa macho atakujibu ni Arsenal.
Lipumba amesema yeye ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal, licha ya klabu hiyo ya England kutotwaa mataji makubwa kwa muda mrefu lakini bado haipunguzi mapenzi yake kwa klabu hiyo ya Ligi kuu England.
Naishabikia Arsenal japo kuwa haifanyi vizuri, lakini ndio timu yangu ninayoipenda,”Alijibu Prof. Lipumba kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV leo asubuhi alipoulizwa ni klabu gani ya mpira wa miguu anaishabikia.
Lipumba pia aliendelea kujinadi kwa kusema, ameshawahi kusukuma kabumbu miaka ya nyuma wakati akiwa mwanafunzi wa shule ya sekondari “ Nimeshawahi kucheza mpira kipindi wakati nasoma sekondari, lakini sio katika ngazi ya ushindani,”.

0 Responses to “Mimi ni shabiki wa Arsenal japo haifanyi vizuri – Prof. Lipumba”

Post a Comment

More to Read