Thursday, September 14, 2017
Kevin De Bruyne amjaza kiburi Pep Guardiola
Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amemsifia
bila kificho kiungo Kevin De Bruyne, kufuatia kazi nzuri aliyoionyesha
usiku wa kuamkia leo wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
dhidi ya Feyenoord.
Guardiola alimwagia sifa kiungo huyo kutoka nchini Ubelgiji mbele ya
waandishi wa habari, mara baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa
mabao manne kwa sifuri katika uwanja wa Etihad Stadium.
Meneja huyo kutoka nchini Hispania alisema, De Bruyne amekua msaada
mkubwa kwenye kikosi chake na anajivunia kuwa na mchezaji wa aina hiyo.
“Kevin ni mmoja wa wachezaji bora nilionao kwa sasa, sikuwahi kuwa na
mawazo tofauti dhidi yake, zaidi ya kuamini anafanya kazi kwa ajili ya
kuisaidia Man City kufikia lengo la kupata ushindi kwenye kila mchezo
tunaocheza, ni faraja kwangu na kwa wengine klabuni hapa.”
Guardiola pia akazungumzia umuhimu wa kikosi chake kupata ushindi
kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu
walioucheza nyumbani kwa kusema, anaamini hatua hiyo itawasaidia katika
safari yao ya kupambana kwenye michezo ijayo.
“Msimu uliopita hatukubahatia kushinda michezo ya ugenini, kwa hatua
hii ya kuanza kupata ushindi nyumbani naamini itatusaidia ili
kufanikisha mpango wa kupambana tutakapokua nje ya Etihad Stadium ili
tushinde na michezo ya ugenini.
“Tumekua na kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya Feyenoord na
tulibahatika kufunga katika dakika ya kwanza ya mchezo, hii inaonyesha
safu yetu ya ushambuliaji ipo makini na tayari kwa wakati wowote kufanya
kinachotarajiwa na wengi. Tuna mambo mengi ya kufanya katika michuano
hii msimu huu, lakini kuanza na ushindi usiku huu ni jambo jema sana
kwetu.
Mabao ya Man City katika mchezo dhidi ya Feyenoord yalifungwa na John
Stones aliyefunga mawili, Sergio Aguero, Kevin de Bruyne na Gabriel
Jesus.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.
Kundi E
Liverpool 2 – 2 Sevilla
Maribor 1 – 1 Spartak Moscow
Kundi F
Feyenoord 0 – 4 Manchester City
Shakhtar Donetsk 2 – 1 SSC Napoli
Kundi G
FC Porto 1 – 3 Besiktas
RasenBallsport Leipzig 1 – 1 Monaco
Kundi H
Real Madrid 3 – 0 APOEL Nicosia
Tottenham Hotspur 3 – 1 Borussia Dortmund
8:45 AM by Unknown · 0
Lema: Lissu bado yupo ICU
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa hali ya
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu sasa inaendelea vizuri
ukilinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali ingawa bado yupo ICU.
Ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na BBC ambapo amedai
kuwa hali ya kiongozi huyo inazidi kuimarika ukilinganisha na siku za
awali ambazo alikuwa amefanyiwa shambulio hilo.
“Mgonjwa anapokuwa yupo hospitali tena kwenye chumba cha wagonjwa
mahututi huwezi kusema hali ya mgonjwa ni nzuri, lakini kwa kadri
ambavyo tumekuwa hapa Nairobi kwa siku zote mimi na wenzangu akiwepo
Mchungaji Msigwa, mke wa Lissu na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe tunaweza
kusema kuna mabadiliko lakini bado Tundu Lissu yupo ICU na ni wito wetu
kwamba Watanzania wote wenye mapenzi mema waendelee kumuombea,” amesema
Lema
Aidha, amesema kuwa jaribio la kutaka kumuuwa Lissu ni mpango na watu
waliofanya hivyo wala siyo majambazi bali walifanya hivyo kwa lengo la
kutaka kutuma ujumbe kuwa wanaweza kufanya lolote na wasifanywe
chochote.
Hata hivyo, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana
Septemba 7, 2017 akiwa Mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya
kwaajili ya kupatiwa matibabu
8:42 AM by Unknown · 0
“Tanzania ipo Salama na Imara” – Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Iran. Mousa Farhang nakufanya mazungumzo ya kikazi leo Septemba 13/2017.Ofisini kwake Magogoni Dar es salaam.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam.
“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.”
Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi.
Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano.
Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Iran ili waje kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.
Pia amewakaribisha raia wa Iran kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.
Kwa upande wake, Balozi Farhang ameipongeza Serikali kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi na kupambana na dawa za kulevya na ufisadi.
Balozi huyo amesema Serikali ya Irani ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na vitendo vingine vya kihalifu.
Balozi Farhang ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya Tanzania ifungue Ofisi ya Ubalozi nchini Iran ili kuimarisha uhusiano huo, ambapo Waziri Mkuu amekubali.
Pia Bw. Farhang amesema aliwahi kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro na kusema kwamba ni maeneo mazuri ambayo hajawahi kuyaona tangu azaliwe.
7:38 AM by Unknown · 0
CUF inahitaji maombi- Kumbilamoto
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto amesema kuwa anasikitishwa na chama chake kwani kinakatisha tamaa kutokana na mgogoro unaoendelea hivyo amewaomba wanahabari kutumia weledi na ushawishi ili kutatua mgogoro huo.
Kumbilamoto ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti kupitia Chama cha Wananchi (CUF) amesema kuwa chama hicho kilikuwa ni kimbilio la wananchi wanyonge lakini kwa sasa kimekuwa ni cha kilio kuanzia viongozi mpaka wanachama wenye mapenzi ya dhati.
“CUF inatia huzuni, Inahitaji maombi ili migogoro iishe, nawaonea huruma sana viongozi hasa madiwani ambao huu mgogoro unawaumiza kwa sababu ni siku chache tu zilizobaki kufikia uchaguzi mkuu wa 2020 kama hawajafanya kitu ni ngumu sana kuja kuwashawishi tena wananchi wawachague,”amesema Kumbilamoto.
Aidha, amesema kuwa mgogoro huo umekivuruga chama ambacho kilikuwa kimbilio la wengi lakini kwa sasa kimekuwa chama cha kulia lia na kutapa tapa sababu ya mgogoro ambao umekuwa ni sumu ndani ya chama hicho.
Vile vile amewaomba waandishi wa habari kusaidia kutatua mgogoro huo kwa kutumia kalamu zao pamoja na hekima zao kufikisha ujumbe kwa jamii na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Hata hivyo, mbali na hayo kiongozi huyo amesema hana mpango wa kuendele kung’ang’ania madarakani endapo pale umri wake wa kuwa kwenye siasa utakuwa umekwenda na kwamba atahitaji mapumziko kwani kiongozi mwenye nia ya kutumikia wananchi huwa haoni utamu wa uongozi.
7:32 AM by Unknown · 0
Wednesday, September 13, 2017
Mugabe amzuia msanii wa kike kuingia Zimbabwe kwa kutovaa nguo za ndani
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameripotiwa kumpiga marufuku
mtumbuizaji wa kike wa Afrika Kusini, Zodwa Wabantu kutumbuiza nchini
humo kutokana na tabia yake ya kupanda jukwani bila kuvaa nguo za ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua kituo
cha taarifa za jamii cha Bindura nchini humo (Bindura Community
Information Centre) hivi karibuni, Rais Mugabe alisema kuwa amemzuia
Zonda kwakuwa vitendo vyake vya kupanda jukwaani bila nguo ya ndani
haviendani na maadili ya nchi hiyo.
Mugabe aliwaomba radhi wanaume ambao alidai kuwa amesikia wakilalamika kuhusu uamuzi huo.
“Hatutaki mtu yeyote msumbufu kuja nchini kwetu akiwa mtupu kwa ajili
ya kusababisha matatizo. Nini hasa lengo lake la kuja hapa? Rais
Mugabe alihoji.
“Ili wanaume waweze kukuona? Poleni. Tumewaangusha wanaume wengi
ambao walikuwa wanalalamika. Nimesikia walikuwa wanataka [Zodwa] aje.
Hayo ni mawazo ambayo hatuyataki, acha hayo yafanyike huko anakotoka
(Afrika Kusini),” anakaririwa na mtandao wa Zimbabwe wa Bulawayo24.

Zodwa Wabantu
Zodwa ambaye ni mtumbuizaji maarufu anayepanda jukwaani akiwa na nguo
zake isipokuwa nguo za ndani, alikuwa amealikwa kushiriki tamasha
maarufu la kimataifa jijini Harare la ‘Harare International Carnival’.
Vyombo vya habari vya Zimbabwe vimeeleza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Maadili ambaye pia ni Waziri wa zamani wa nchi hiyo, Aeneas Chigwedere
alisema kuwa vitendo vya Zodwa ni kinyume cha maadili na kwamba uamuzi
wa Serikali umelenga kuwalinda vijana na jamii kwa ujumla dhidi ya
kumomonyoka kwa maadili.
Tamko la Serikali hiyo lilitolewa muda mfupi baada ya baadhi ya
wasanii wa nchi hiyo kulalamikia kitendo cha waandaaji wa tamasha hilo
kutaka kuwatumia zaidi wasanii wa nje ya nchi na kuwaacha wasanii wa
ndani.
7:34 PM by Unknown · 0
Bunge laziunganisha TRL na RAHCO

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada
wa sheria ya reli ya mwaka 2017 (The Railways Act, 2017) ambao
unapendekeza kuanzisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) litakalokuwa na
jukumu la kusimamia, kuendeleza miundombinu ya reli na kutoa huduma ya
usafiri wa reli.
Hayo yamesemwa hii leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akiwasilisha
muswada huo, ambapo amesema kuwa dhumuni ya muswada huo ni kuweka mfumo
madhubuti wa utoaji huduma ya usafiri wa reli, usimamizi na uendelezaji
wa miundombinu ya reli.
“Muswada huu unaainisha utaratibu wa kuhamisha watumishi kutoka
(Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli
Nchini (RAHCO) kwenda katika Shirika jipya,” amesema Prof. Mbarawa.
Amesema kuwa muswada huo pia unaainisha vyanzo vya mapato ambavyo ni
pamoja na mfuko wa reli, ruzuku toka Serikalini, nauli za abiria pamoja
na uhifadhi wa eneo la reli.
Prof. Mbarawa ameongeza kuwa TRL ilikuwa ikisimamia masuala ya
usafiri wa gari moshi (treni) na RAHCO ilikuwa ikisimamia miundombinu,
kwa kipindi chote ambacho taasisi hizo zimetenganishwa katika utendaji
kazi kumesababisha kushuka kwa mapato na utendaji wa TRL.
Hata hivyo, amesema kuwa, Serikali imechagua Shirika kuitwa TRC
kutokana na namna ambavyo Watanzania waliliamini shirika hilo kabla ya
kubadilishwa jina kwenda TRL ambapo kumekuwa na changamaoto
nyingi ikilinganishwa na hapo awali.
7:31 PM by Unknown · 0
Lady Jay Dee amvuta tena Justin Campos

Msanii Lady Jay Dee amvuta tena kwa mara nyingine muongozaji
wa video kutoka nchini Afrika ya kusini ‘Justin Campos’ katika nyimbo
yake mpya ya ‘I Miss You’ ambaye ndio ameifanya video ya wimbo huo.
Lady jay Dee ameeleza kuwa video yake ya nyimbo ya I Miss You
imefanywa nchini Afrika ya Kusini na mtayarishaji akiwa ni Justin Campos
ambaye ndiye aliefanya video yake ya nyimbo iliyofanya vizuri ‘Ndi ndi
ndi’ nyimbo ambayo mpaka sasa inajumla ya watazamaji zaidi ya milioni 1
katika mtandao wa YouTube.
‘’Video ya nyimbo yangu mpya I Miss You itatoka Ijumaa hii na video
imeongozwa na mtayarishaji Justin Campos kutoka nchini Afrika Kusini
ambaye ndio alie fanya video yangu ya Ndi ndi ndi’’ amesema Lady Jay
Dee.
Nyimbo ya I Miss You ndio kazi ya kwanza kwa msanii Lady Jay Dee
tangu alipotoa Album yake ya Saba ‘Women’ album iliyotoka mwaka huu.
7:30 PM by Unknown · 0
BUNGENI BALAA: SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AMCHIMBA MKWARA MZITO ZITTO KABWE
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amesema ana uwezo
wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzungumza mpaka mwisho wa bunge,
kwani hawezi kupambana naye.
Spika
Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi
kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa
Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda
wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na
muda wake kuliongoza bunge hilo.
"Hawa
ni watu nawaheshimu sana na wamenilea sana na ni sehemu nilipofika hapa leo.
Utanilinganishaje mimi na milima mikubwa kama Kilimanjaro? Hata siku moja sikio
haliwezi kuzidi sikio," amesema.
Amesema
katika Bunge la 9 Zitto aliwahi kupeleka hoja ya Mgodi wa Buzwagi ambayo
ilikataliwa na Bunge lakini ikazuka hoja ya kimaadili ambapo alihukumiwa hapo
hapo.
"Alihukumiwa
hapo hapo akapigwa miezi mitatu. Mnataka niende mkuku mkuku kama lile la Bunge
la tisa nifanane na mzee Sitta? Hilo pia naliweza kwa nini mnaalika matatizo
nashangaa unapambana na Spika," amesema.
"Ninauwezo
wa kupiga marufuku kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe hauna pa kwenda,
hakuna cha swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya nini?
Amemtaka
kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.
"Kwa
haya ya Spika sina sababu nayo lakini ya kulidharau Bunge hayo sitaweza
kuyavumilia nitalinda mihimili huu kwa nguvu zangu zote," amesema.
Amesema
hawawezi kuacha wabunge kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba watachukuliaje
Watanzania wengine watakapolidhalilisha Bunge.
Amesema
hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
"Tutaenda
sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke," amesema
Hapo
jana Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa
maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa
mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge
2:46 PM by fahari news · 0
Petr Cech awataka wenzake kupambana kama Chelsea
Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech, ambaye aliwahi kutwaa
ubingwa wa Europa league akiwa na Chelsea, amewataka wachezaji wenzake
kupambana kufa na kupona ili kufanikisha mpango wa kufanya vyema kupitia
michuano hiyo ya barani Ulaya.
Amesema: “Tunapaswa kuchukua maamuzi ya kupambana kwa vyovyote vile, ili tufikie lengo.
“Nilipokua Chelsea, kila mmoja wetu alisikitishwa na hatua ya
kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi, lakini
tulipoanza kushiriki Europa League kila mmoja alijitoa kwa hiyari yake
na tukafanikiwa kutwaa ubingwa, ninaamini suala hilo linawezekana nikiwa
Arsenal.
“Jambo kubwa ni kujikubali na kutambua unapambana kwa lengo la
kufanya vyema, nimeshawahamasisha wenzangu kwa kutaka kuona suala hilo
linatokea ili iwe furaha kwetu sote mwishoni mwa msimu.”
Arsenal wanashiriki michuano ya Europa League, kutokana na kumaliza
katika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ya nchini England msimu wa
2016/17.
8:26 AM by Unknown · 0
Rufaa ya Sadio Mane yagonga ukuta
Mshambuliaji wa majogoo wa jiji Liverpool Sadio Mane
ataendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu, baada ya rufaa ya
kupinga kadi nyekundi aliyoonyesha mwishoni mwa juma lililopita, kuwekwa
kapuni na chama cha soka nchini England (FA).
Mane alionyeshwa kadi hiyo baada ya kumpiga teke la uso mlinda mlango
wa Man city Ederson, katika mchezo wa ligi ya nchini England ambao
ulimalizika kwa Liverpool kukubali kufungwa mabao matano kwa sifuri
kwenye uwanja wa Etihad.
FA wamejiridhisha kwa kurejea picha za video za mchezo huo, na
kubaini mwamuzi Jon Moss alichukua maamuzi sahihi ya kuuadhibu
mshambuliaji huyo kutoka nchini Senegal, kutokana na kosa alilolifanya.
Hata hivyo meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado ameendelea kupingana
na maamuzi hayo, kwa kusema Mane hakukusudia kumuumiza Ederson, bali
kitendo kilichotokea kilikua bahati mbaya.
Kwa mantiki hiyo Mane atakosa mchezo dhidi ya Burnley utakaochezwa
mwishoni mwa juma hili. Pia atakosa michezo miwili dhidi ya Leicester
City ya kombe la ligi na ligi ya England.
8:23 AM by Unknown · 0
AudioMPYA: Rayvanny ameachia wimbo mpya ‘Unaibiwa’
Msanii wa Bongofleva kutoka record label ya WCB Rayvanny leo September 12 2017 ameachia audio ya ngoma yake mpya iliyofanywa na producer wao Lizer kutoka record labe ya WCB wimbo unaitwa ‘Unaibiwa’
8:11 AM by Unknown · 0
Serikali kununua mashine za DNA
Serikali
imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili
zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na
wananchi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na
Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni,
Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli
ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.
Amesema
kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha
uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa
ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
”
Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi
kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja
kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo
wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa
namna stahili,” amesema Dkt. Kigwangala.
Aidha,
amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka
maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi
kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo cha kupima
vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza ucheleweshaji wa
matokeo ya uchunguzi
6:57 AM by Unknown · 0
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 13, 2017

6:53 AM by Unknown · 0
Subscribe to:
Posts (Atom)
.gif)









