Thursday, March 6, 2014
PINDA ATETA NA WAPINZANI
Do you like this story?
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda
amelazimika kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani kunusuru majadala wa
kanuni za bunge umalizike salama.
Kikao hicho kilifanyika
juzi baada ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge saa 3 usiku hadi 6. Pinda
aliwasihi viongozi hao watumie kila aina ya busara mjadala huo wa umalize
salama na kila upande kuridhia kanuni hizo kupita.
Viongozi alikuwana nao
pinda kwa faragha ni kiongizi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa CUF ambaye pia ni mjumbe wa bunge maalumu la katiba,
Profesa Ibrahim Lipumba.
Katika kikao
hicho kilichofanyika katika ofisi ya wziri mkuu katika ofisi ya bunge pinda
alitumia muda mwingi kuwataka viongizi hao kutanguliza maslahi ya taifa katika katiba inayokusudiwa iweze
kupatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PINDA ATETA NA WAPINZANI”
Post a Comment