Thursday, March 6, 2014

SH MIL 600 KUTUMIKA KIAPO KWA WAJUMBE


Bunge la Katiba


MJUMBE wa bunge la katiba, Ali Kessy amepinga utaratibu wa kuapishwa mjumbe mmoja mmoja kwa bile zitatumika zaidi y ash milioni 600 kwa kazi  hiyo.

Hayo aliyasema juzi jioni mjini hapa wakati akichangia mjadala wa kanuni ya 10 (3) ya bunge maalum la katiba.

Amesema suala la kuapa kwa mtu mmoja  mmoja ni kuongeza gharama  kwa serikali na kutumia vibaya kodi za wananchi.

“Serikali inaweza kutumia zaidi ya sh milioni 191 kwa siku kama posho kwa wjumbe wote hivyo endapo wajumbe hao wataapishwa kwa siku tatu zaidi y ash milioni 600 zitatumika .

“Mimi nafikiri ni vema tukaapa kwa pamoja lakini kuapa kila mtu peke yake ni kutumia vibaya kodi za wananchi wetu “alisema kessy”

Hoja hiyo ya kessy iliungwa mkono na mjumbe Freeman Mbowe ambaye naye alisema utaratibu  wa kuapa mmoja mmoja ni kuongeza gharama kwa serikali.

Amesema ni vema utaratibu ukawekwa wajumbe hao waape kwa pamoja kupitia makundi kuokoa fedha za serikali na hasa za kodi za wananchi.

Mjumbe Ezekiah Oluoch alisema yeye binafsi alishawahi kuw ambunge wa bunge la Africa na waliwahi kuapishwa kwa utaratibu mmoja.

0 Responses to “SH MIL 600 KUTUMIKA KIAPO KWA WAJUMBE”

Post a Comment

More to Read