Thursday, March 6, 2014

ROSTAM WAPILI KWA UTAJIRI AFRIKA MASHARIKI.


Rostam Aziz


MFANYABIASHARA Rostam Aziz anaedelea kutajwa kuwa tajiri namba moja katika Tanzania akimiliki utajiri wa dola za marekani bilioni moja , huku akishika nafasi ya 27 kati ya matajiri wa Africa  na namba 1565 duniani.

Kwa mujibu wa jarida la biashara la hivi karibuni la Forbes, Rostam Aziz mwenye umri wa miaka 45 anamiliki utajiri huo unaotokana na uwekezaji katika biashara ya mawasiliano na hisa katika kampuni mbalimbali.

Katika orodha mpya ya matajiri iliyotolewa wiki hii na jarida hilo rostam amekuwa kinara wa utajiri nchini kutokana na kujihusisha na biashara ya mawasilino kwa kumiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya Vodacom yenye zaidi ya wateja milioni 10 kote nchini.

Forbes limesema Rostam anaendesha biashara  za majengo kampuni za madini ya Caspian ambayo inatoa huduma za uchimbaji wa madini kwa kampini za madini za Barrick Gold, na BHP Bilioni , pia ana hisa katika kampuni ya Hutchison Whampoa na anamiliki vyombo vya habari .

Katika orodha ya matajiri wa Africa Mashariki  bilionea Sudhir Ruparelia wa Uganda ndiye anaongoza  akiwa na utajiri wa dola za marekani bilioni 1.1

Mganda huyo utajiri wake unatokana na kumiliki majengo, benki na biashara mbalimbali kupitia kampuni yake ya Ruparelia Group. Ruparelia anamiliki benki ya Crane, Hotel na maelfu ya biashara nchini Uganda akiwa na makazi yake kampala. Pia anamiliki shule mbili za sekondari za Highbrow.

Kwa wanawake matajiri barani Africa Folorunsho Alakaja wa Nigeria ameshika namba moja nchini humo akiwa na utajiri wa dola za marekani bilioni 2.5 pamoja na Afrika kwa ujumla . Mwanamama huyo alianza maisha y ake kwa kuwa katibu muhtasi katika miaka ya 1970 kabla ya kuachana na fani hiyo alikwenda kusomea mitindo nchini uingereza . kwa sasa anamiliki zaidi ya asilimia 60 ya hisa katika kampuni mbalimbali.

0 Responses to “ROSTAM WAPILI KWA UTAJIRI AFRIKA MASHARIKI.”

Post a Comment

More to Read