Thursday, March 6, 2014
MADUDU MAPYA YAIBUKA IPTL.
Do you like this story?
UMEIBUKA mkanganyiko mpya kuhusu taarifa za uuzwa kwa
kampuni ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited(IPTL) sambamba
na kuchotwa kwa fedha zinazokadiriwa kufikia shilingi bilioni 120 kutoka katika
akaunti maalum iliyokuwa benki kuu ya Tanzania.(BOT)
Mkanganyiko huo unatokana
na hatua ya mwanahisa mwanzilishi wa IPTL, James Rugemalira kuibuka na
kuzungumza na waandishi wa habari jijini dare s salaam jana na kutoa taarifa
zinazokinzana na habari ambazo zinakuwa zikiripotiwa katika vyombo vya habari
katika siku za hivi karibuni.
Akizungumzia mzozo huo,
rugemalira amesema mkataba wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya
kufua umeme ya IPTL, hivi sasa
unamalizika mwaka 2022 badala ya mwaka 2015 kama ilivyokuwa awali.
Kauli hiyo ya Rugemalira inakinzana na taarifa
ambazo zilikuwa zikionyesha kwamba katika makubaliano ya awali ya mkataba h uo
wa miaka 20 kati ya IPTL na shirika la umeme Tanzania (TANESCO), ulisainiwa
mwaka 1995 na ulitakiwa kuisha mwaka 2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MADUDU MAPYA YAIBUKA IPTL.”
Post a Comment