Thursday, March 6, 2014
ETOILE YAIBUKA UPYA SAKATA LA OKWI.
Do you like this story?
Emmanuel Okwi |
SAKATA la usajili wa
Mganda Emmanuel Okwi Kutua yanga limeibuliwa tena na timu yake ya awali
iliyokuwa ikimmiliki ya Etoile du sahel ya Tunisia baada ya ya kuifungulia
madai ya fidia timi ya SC villa ya Uganda ya Euro milioni 1 (sawa n ash
Billioni 2.2) za kitanzania kwenye shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) kwa
kosa la kumuuza mchezaji wao huyo.
Desemba 14 mwaka jana vila
ilimuuza mchezaji huyo kwenda yanga ambaye kwa sasa ameshaichezea yanga mechi
mbili za mashindano na kufunga bao moja , mechi hizo ni ile ya ligi kuu ya
Vodacom (VPL) dhidi ya ruvu shooting waliyoshinda mabao 70 pia ya ligi ya
mabigwa Afrika dhidi ya Al Ahyl ya misri na kushinda bao 1-0
Kwa mujibu wa chanzo cha
ndani ya timu ya simba kinaeleza kuwa wametumiwa barua na FIFA kuwataarifu juu
ya timu hiyo kufungua madai hayo baada ya mchezaji huyo kuanza kuitumikia rasmi
yanga bila wao kuhusishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ETOILE YAIBUKA UPYA SAKATA LA OKWI.”
Post a Comment