Thursday, March 6, 2014

FUIME AENDELEA KUSOTA RUMANDE


Mkurugenzi wa zamani wa manispaa ya ilala Gabriel Fuime


Upelelezi wa kesi ya mauaji ya watu wane inayomkabili mkurugenzi wa zamani wa manispaa ya ilala Gabriel Fuime (61) bado haujakamilika , mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu jijini dare s salaam iliambiwa jana.

Kutokana na upelelezi kutokamilika hakimu mkazi Augustina Mmbando alimaua kuahirisha kesi hiyo hadi machi 12 2014 mwaka huu.

Mahakama ilielezwa kuwa kesi hiyo ilipelekwa kortini hapo kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi wake ungekuwa umekamilika ili hatua nyingine ziendelee .

Mkurugenzi huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka manne ya mauaji anayodaiwa kuyafanya machi 29 ,2013  mwaka jijini dare s salaam .

Katika shtaka la kwnaz anatuhumiwa kumuua kwa makusudi Gabriel Kamwela kaeneo ya mtaa wa indira gandh wilaya ya ilala.

Aidha ililezwa mahakamani hapo kuwa shtaka la pili linalomkabili mtuhumiwa ni mauaji ya mtu mwingine aliyetajwa kwa jina la philipo kusimala. Aliyoyafanya siku ya tukio la kwanza mtaaani hapo.

Iliendelea kudaiwa mahakamani kuwa shataka la tatu pia ni la mauaji ya mwingine aliyetajwa kwa jina la bethod mwanengule. Mtaani hapo.

Katika shtaka la nne mtuhumiwa anadaiwa kufanya mauaji ya mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la zahda kanji.

Baada ya kusomewa mashtaka mtuhumiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa vile kisheria mahakama ya hakimu mkazi kisutu haina mamlaka ya kuyasikiliza mashtaka mauaji zaidi ya mahama kuu.

0 Responses to “FUIME AENDELEA KUSOTA RUMANDE”

Post a Comment

More to Read