Friday, March 7, 2014

WAZOMEAJI BUNGENI KUKIONA CHA MOTO.




Wajumbe wa bunge maalumu la katiba wameafiki kuongezwa kwa vipengele katika kanuni za uendeshaji wa bunge hilo vitakavyowabana wajumbe wenye tabia ya kuwazomea wenzao.

Kanuni hiyo itawabana pia wajumbe wenye tabia ya kuwadhihaki na kwaudhi wenzao wakati wanpochangia mijadala.

Hatua hiyo imekuja wakati tabia hizo zimeanza kujitokeaza miongoni mwa wajumbe.

Uamuzi kuhusu kuongezwa kwa kipengele hicho ulitangaza juzi na mjumbe wa kamati ya kupitia rasilimu za kanuni za bunge hilo, evod mmanda wakati wakitoa ufafanuzi.

Ufafanuzi huo uliotokana na baadhi ya wajumbe kueleza kukerwa kwao na tabia hizo.

“Hakuna uhusur usiokuwa na mipaka,tusipotengeneza kanuni zetu vizuri kuna watu watatumia uhuru vibaya kwa kukashifu wengine amesema mmanda.

Mmanda alishauri kuwa ni lazima kiwekwe kifungu cha kuwazuia watu kudhalilisha wenzao na hata viongozi.

“Mimi napenda uhuru lakini uhuru usiokuwa na kikomo ni vurugu” aliongeza.

0 Responses to “WAZOMEAJI BUNGENI KUKIONA CHA MOTO.”

Post a Comment

More to Read