Friday, March 7, 2014
MVUA ZAWAWEKA ROHO JUU WAKAZI DAR.
Do you like this story?
Dar es salaam |
Mvua zinazoendelea
kunyesha jijini dar es salaam, zimezua taharuki kwa wakazi wake hasa baada ya
kusababisha athari katika baadhi ya maeneo muhimu.
Moja ya maeneo hayo ni
hospitali ya palestina iliyopo sinza ambayo ilijaa maji na kusababisha usumbufu
mkubwa.
Mganga mkuu wa hospitali
hiyo . DK benedict luoga amesema mvua hizo zilizonyesha juzi zilisababisha maji
kuingia katika moja ya majengo yake.
Amesema kutokana na hali
hiyo, shughuli katika hospitali zilisimama kwa muda hadi kazi za kutengeneza
njia mbadala ilipokamilika.
“Tumeshapeleka malalamiko
yetu kwenye mamlaka husika lakini hakuna kinachofanyika. Tulichoamua kufanya
sasa ni kujenga tuta la kingo ili kuziua maji yaiingie ndani hasa katika kipindi
hiki ambacho mvua zinaendela kunyesha” alisema .
Katika maeneo mbalimbali
ya jiji hilo baadahi ya barabara na mifereji ya maji machafu ilionekana ikiwa
imejaa maji na kusababisha foleni kutoka na madereva kuendesha magari kwa
tahadhari.
Baadhi ya maeneo
yaliyoathiriwa na mvua hizo ni vingunguti, sinza, kipawa, jangwani,kariakoo na
kigogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MVUA ZAWAWEKA ROHO JUU WAKAZI DAR.”
Post a Comment