Friday, March 7, 2014
MUHONGO AONGEZA UTATA MABILIONI YA IPTL.
Do you like this story?
Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo |
Wakati utata wa kuchotwa
kwa fesha katika akaunti ya Escro iliyofunguiwa katika benki kuu ya Tanzania (BoT)
kutokana na mgogoro baina ya IPTL na Tanesco ukiendelea kuzua maswali, waziri
wa nishati na madini profesa Sospeter muhongo amesema fedha hizo hakzikuwa za
serikali.
“Hizo fedha hazikuwa za
serikali, Tanesco ilitakiwa kulipa Capacity charge(gharama za uwekezaji) kwa
IPTL kama inavyolipa karibu sh 27 billioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha
umeme” alisema profesa muhongo.
Itakumbukwa kuwa
kutokana na mgogoro wa IPTL na Tanesco
akaunti hiyo ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa kulipa IPTL kwa
ajili ya capacity charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo hadi mgogoro huo
utakapomalizika.
Kwa kuwa malalamiko
yalikuwa kwamba, fedha Ambazo Tanesco ilikuwa ikiilipa IPTL zilikuwa nyingi
kuliko ilivyostahili, ilitarajiwa kwamba baada ya kesi iliyofuguliwa marekani kuamuriwa,
ingepatikana njia kukokotoa gharama halisi na sehemu ya fedha hizo kurudi
Tanesco.
Sehemu ya taarifa kwa umma
iliyotolewa na ofisi ya uhusiano Tanesco Makao makuu jumanne iliyopiga
kufafanua taarifa zilizokuwa zimeandikwa juu ya hukumu hiyo inasema mahakama
hiyo (ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji) haikutangaza
aliyeshinda wala kushindwa
Ilichofanya ni kutoa muda
wa miezi mitatu pande zeote mbili,(standard chartered bank) Hong
kong(SCB-HK) na Tanesco kwenda
kukubaliana nje ya mahakama kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu
taratibu za kukokotoa gharama halisi.
Profesa muhongo
alipoulizwa iwapo serikali inaitambua SCB- HK na hukumu iliyotolwa na mahakama
hiyo ya kimataifa alisema kwa kifupi “kwani sisi tunaendeshwa na sheria za
marekani?he gai wabia wengine wanatambua SCB-HK?
Pia hakutaka moja kwa moja
kukiri kuwa serikali ndiyo iliyotoa fedha hizo na kuzitoa kwa pan African power
solution wala kukanusha taarifa hizo, badala yake alisema swali hilo waulizwe
wahusika katika suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MUHONGO AONGEZA UTATA MABILIONI YA IPTL.”
Post a Comment