Thursday, March 6, 2014

SIMBA YAKANA KUNG’OA VITI




Uongozi wa klabu ya simba umesema hauhusiki na vurugu zilizotokea katika medhi ya yanga dhidi Al Ahly uliochezwa jumapili iliyopita kwa sababu hawakuwa na masilahi na mechi hiyo.

Afisa habari wa simba asha muhaji alisema mashabiki waliofanya vurugu zile ni wa  Al Ahyl  na wala siyo wa simba kwa kuwa mechi ile iliwahusu yanga na ahyl na siyo simba.

Waliofanya vile ni mashabiki wa al ahyl kwani ndiyo waliokuwa wapinzani wa yangua siku hiyo kwnza inashagaza simba tunahusikaje katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo? Alihoji muhaji

Akizungumza kigezo cha wahusika wa kuvaa jezi zenye rangi nyekundu inayotumiwa na klabu ya yake alisema si kweli simba ndiyo inatumia jezi zenye rangi nyekundu pekee.

Wakati huo huo serikali imesema inafanya tathimini ya uharibufu ambao umefanyika kwenye mchezo baina ya yanga na al ahyl mwishoni mwa wiki iliyopita kabla ya kuangusha rungu lake.

Naibu waziri wa habari,  vijana utamaduni na michezo juma nkamia alisema shirikisho la soka Tanzania (TFF) ndio liliomba kutumia uwanja huo kwa hiyo kesho watakutana na viongozi wa TFF ili gharama za uharibifu wa mali za uwanja ziweze kufidiwa.

0 Responses to “SIMBA YAKANA KUNG’OA VITI”

Post a Comment

More to Read