Thursday, March 6, 2014
KESI YA MBUNGE WA BAHI YACHUKUA SURA NYIGINE
Do you like this story?
Dar es salaam. Kesi ya kuomba na kupokea rushwa
inayomkabili mbuge wa bahi (CCM) omary badwel katika mahakama ya hakimu mkazi
kisutu imeahirishwa hadi april 4 kwa
ajili ya kutolewa uamuzi kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa ama la.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mbunge huyo kufungua kesi
ya kikatiba mahakama kuu hivyo mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi wa kesi
kuendelea kusikilizwa ama kusitishwa kwa ajili ya kusubiri uamuzi utakaotolewa
mahakama kuu.
Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo june 4 2012
ambapo alidaiwa kuomba rushwa y ash 8 milioni kutoka kwa aliyekuwa mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya mkuranga , sipora jonathan liana.
Kwa mujibu wa kesi hiyo mbunge huyo anadaiwa kutenda kosa
hilo kwa nyakati tofauti kati ya mei 30
na juni 2 2012 katika maeneo tofauti ya d res salaam akipokea rushwa ya
sh 1 millioni kutoka kwa mkurugenzi wa zamani wa halmashauri hiyo mkuranga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KESI YA MBUNGE WA BAHI YACHUKUA SURA NYIGINE”
Post a Comment