Thursday, March 6, 2014

MTOTO WA MIAKA 13 ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI




Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi majengo, wilayani kahama, mkoani shinyanga amelazwa katika hospitali ya wilaya baada ya kunusurika kifo kutokan ana jaribio la kuchinjwa na baba yake mzazi.
“ Tukio hilo limekuja siku 10 baada ya mtu mmoja, ustadhi Mohamed Kurangwa(36), kumuua mwanafunzi wa shule ya msingi Nzasa, Jamal Salum(12) kasha naye kuuawa, Mbagala, Dar es salaam .

Kurangwa alimuua Jamal nyumbani kwake Mbagala Charambe mianzini kwa kumchinja na kweka kichwa cha marehemu kwenye miguu yamtoto huyo , kasha kuupeleka mwili wake choo cha nyumba anayoishi muuaji.

Muuaji huyo alizoa damu na kujaza kwenye ndoo kasha kuiweka pembeni ya nyumba yake kabla ya kuingi chumbani kwake, kujifungia na kusoma Koran. Katika tukio la kahama, Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo DK Joseph Fwoma alimtaja Mwanafunzi huyo kuwa ni said siraji(13) na alifikishwa hospitalini hapo jana alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akivuja damu shingoni.

DK Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini, madaktari wamfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyokatwa na hadi jana alasiri hali yake ilikuwa inaendelea vizuri baada ya kuongezwa damu.

0 Responses to “MTOTO WA MIAKA 13 ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI”

Post a Comment

More to Read