Thursday, March 6, 2014

WACHINA WATOA RUSHWA


Mahakama ya kisutu


Rais wa China Huang Gin, Xu Fujie na Chen Jinzha wamedaiwa kutoa hongo y ash 30.2 milioni kwa polisi na askari wa wanyamapori ili wasipekue nyumba waliyokuwa wakiishi iliyo mtaa wa kifaru Mikocheni.

Washitakiwa hao wanadaiwa kukutwa na nyara za serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 1.880 vyote vikiwa na thamani ya sh 5.4 bilioni.

Shahidi wa upande wa mashtaka,ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana na amri ya hakimu Isaya Arufani wa mahakama ya Hakimu Mkazi wa kisutu iliyotolewa jana ya kuvitaka vyombo vya habari kutotaja majina ya mashahidi watakaotoa ushahidi kwenyekesi hiyo, alidai kushuhudia tukio hilo.

Alidai kuwa wakati wakiendelea kufanya upekuzi kwenye nyumba waliyoukuwa wakiishi washtakiwa hao, Huang Gin alivuta droo na kutoa bahasha iliyokuwa na fedha ndani ambazo walizihesabu zilikuwa ni sh 30.2 milioni kama kishwawishi cha kuwataka wasiendelee kuipekua nyumba hiyo.

“Hatukukubaliana na ofa hiyo kwa sababu tuliamini kuna kitu ndani yake na ni lazima tufanye upekuzi na kiasi hicho cha fedha tukakichukua kama kielelezo cha ushahidi “, alidai shahidi huyo.

0 Responses to “WACHINA WATOA RUSHWA”

Post a Comment

More to Read