Sunday, December 8, 2013



RAISI OBAMA, CLINTON, BUSH KUELEKEA AFRIKA KUSINI


Rais wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama watasafiri wiki ijayo kuelekea Afrika Kusini kushiriki Mazishi ya Nelson Mandela. Taarifa kutoka ikulu kwa msemji wa ikulu ya Marekani Jay Carney imesema Obama na Mkewe wataenda kwenye Mazishi lakini haijafahamika kwamba Obama ataenda siku gani kati ya tarehe 10 Disemba au siku ya Maishi tarehe 15 disemba.

Aidha Rais Mstaafu wa Marekani George W. Bush ofisi yake imesema Bush atasafiri na Obama katika Ndege ya Air Force One kuelekea kwenye mazishi ya Nelson Mandela. Obama pia amemuarika baba wa Raisi huyo mstaafu H.W Bush lakini hawezi kwenda kutokana na umri wake wa miaka 89 kutomuwezesha kusafiri umbali mrefu.


Clinton ameiambia CNN kuwa ataenda na mkewe katika mazishi ya Nelson Mandela lakini bado haijafahamika ni lini na kama ataambatana na Obama pamoja na Bush kwenye msafara huo.


   

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read