Saturday, March 1, 2014

OMEGA SEME ARUDI TENA YANGA


MCHEZAJI WA TANZANIA PRISONS OMEGA SEME
MCHEZAJI  kiungo wa Timu ya Tanzania Prisons Omega  Seme, amesema anafurahia kurudi tena kwenye timu yake ya zamani ya  Yanga  mara mzunguko wa pili wa ligi kuu utakapomalizika.
 
Seme, ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na  Fahari News  mara baada ya kumaliza mazoezi  ya asubuhi kwenye uwanja wa timu ya Tanzania Prisons, licha ya kushindwa kuweka wazi  usajili wake huo   kwa klabu ya Yanga Africans.
 
Amesema, mchezaji anapochezea klabu kubwa kama Yanga, Simba na Azam anakuwa na uwezo mkubwa  na ujuzi wa kiuchezaji tofauti na timu ndogo.
“Kweli nimekubali kurudi tena kwenye timu yangu ya Yanga ile ni timu kubwa hivyo nitapata ujuzi zaidi  kutokana na kucheza mechi nyingi tofauti na sasa,”amesema.
 
Aidha, amesema licha ya kwamba anatarajia kuondoka kwenye  timu hiyo ya  Tanzania Prisons mara ya kumalizika kwa mashindano hayo ya ligi kuu lakini  anamatumaini makubwa  na kikosi hicho kufanya vizuri zaidi kutokana na mikakati mizuri ya kocha wao Mwamwaja

0 Responses to “OMEGA SEME ARUDI TENA YANGA”

Post a Comment

More to Read