Tuesday, April 8, 2014

MAJAMBAZI YAUA, YATEKA MAGARI YA MAGAZETI.




Morogoro. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga na kupigwa na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi

Ambao walifunga Barabara ya morogoro- iringa,eneo la mkata, Doman a kuteka magari kisha kupora mali na fedha za wasafiri.
Miongoni mwa magari yaliotekwa,limo la kampuniya Mwananchi  

Lililokuwa likisafirisha magazeti  kwenda mikoa ya iringa na mbeya na jingine la kampuni  ya Global Publishers ambalo nalo lilikuwa likisafirisha magazeti.

Kaimu  kamanda  wa polisi mkoa wa mor
ogoro,  John laswai alisema tukio hilo la utekaji lilitokea juzi usiku kati ya saa saba na saa tisa usiku. Aliyefariki katika tukio hilo ni  Alex Mgombea (38) ambaye alizama kwenye mto uliopo jirani na eneo hilo wakati majambazi  hayo yalipokuwa  yakimfukuza kwa mapanga na silaha nyingine.
Kaimu kamanda huyo amesema majeruhi wa tukio hilo wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani morogoro na hali zao zinaendelea kuimalika.

Hata hivyo. Alisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba jeshi  la polisi  linaendelea na uchunguzi zaidi.

0 Responses to “MAJAMBAZI YAUA, YATEKA MAGARI YA MAGAZETI.”

Post a Comment

More to Read