Tuesday, April 8, 2014

WABADILI MBINU KUSAFIRISHA ‘UNGA’.





Dar es salaamu. Wakati kitendo cha kudhibiti Dawa za kulevya Tanzania kikiumiza kichwa ni namna  gani kitamaliza wimbi la biashara na matumizi ya dawa za kulevya, wahalifu wamegundua njia mpya za kusafirisha kilevi hicho ikiwamo kuwatumia wanawake wajawazito. 

Imeelezwa kwamba mbali ya kuwatumia wajawazito. Pia hutumia ndege za mizigo kwa kuweka dawa za kulevya kwenye wanasesere au jarida,makopo ya maziwa ya watoto, vinyago na kuzituma kama vifurushi kwenda sehemu nyingine.

Akizungumza jana, kamanda wa kitengo hicho Godfrey Nzowa  amesema wasafirishaji  hao wanawatumia wajawazito kwa sababu  wanawaamini  kuwa hawawezi kukaguliwa kwa mashine kutokana na sababu za kiafya. 

Alisema hali imekuwa ikiwapa wakati mgumu kuwabaini wajawazito wahalifu wanapofika kwenye viwanja vya ndege kwa kuwa hawakaguliwi kwa mashine hizo.
‘’Mwaka 2012 tuliwakamata wajawazito wakiwa wmemeza dawa za kulevya na hadi sasa tunaendelea kuwakamata kwa kupata taarifa kutoka kwenye mataifa tunayo shirikiana nayo katika kupambana na dawa za kulevya,alisema na kuongeza:” kama hatujapata taarifa, mjamzito huyo anapitisha dawa za kulevya kwa sababu hakaguliwi na mashine za X-ray  kwa ajili ya kumlinda mtoto aliye tumboni nah ii ni changamoto kubwa sana,”alisema kamanda Nzowa.

Alisema njia nyingine ni kusafirisha dawa aina ya Cocaine kwa kutumia mfumo wa maji. Alisema wahalifu hao wamekuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kuziweka kwenye makontena huku zikiwa kwenye madumu na chupa wakidai kuwa ni maji.

Alisema njia nyingine inayotumika hivi sasa ni ya watoto wadogo… ‘’Mfano mtuhumiwa aliyekamatwa hivi karibuni na kilo 3.6 za Cocaine alimtanguliza mtoto wake wa miaka saba akidai anakwenda uturukikwa mumewe kumpeleka mwanaye,’’ alisema kamanda Nzowa.

0 Responses to “ WABADILI MBINU KUSAFIRISHA ‘UNGA’.”

Post a Comment

More to Read