Tuesday, April 8, 2014

WAZANZIBAR ‘WAMKUNA’ MTIKILA.








Dodoma. Mjumbe wa Bunge la katiba, Mchungaji  Christopha Mtikila  amewapongeza  Wajumbe kutoka Zanzibari   kwa kutetea haki  za Watanganyika.

Mchungaji Mtikila alisema, chini ya  mwenyekiti Ole Sendeka, wajumbe wa kamati hiyo walikataa mapendekezo mengi  yaliyolenga  kubadili baadhi ya vipengele vya sura ya kwanza na sita  na kusababisha  kukosekana thelathini mbili ya kula kwa upande wa Zanzibar.

Alisema hiyo inamaanisha  mfumo wa rasimu iliyowasilishwa bungeni  na kuanza kuboreshwa na Bunge hilo  Jumatatu,  haukuathiliwa na uamuzi ya kamati hiyo.

‘’Raha niliyoipata kwa Ole Sendeka ni kupewa nafasi ya kuzungumza, nikaitumia kuwafundisha Wajumbe hasa  Watanganyika   Wenzangu kujitambua na kuthamini  utaifa Wao,’’ alieleza  Mchungaji  Mtikila.

Alisema kujitambua na kuifadhi historia ya asili na utaifa wa mtu ni mpango wa uumbaji wa Mungu, ambao hautakiwi kuzuiwa  na yeyote kwa sababu yeyote na kwamba anayelazimisha kuhalibu mpango ni shetani.

Alisisitiza kuwa mchakato wa katiba umethibitishia ulimwengu  kuwa Wazanzibari wanajitambua. Wanathamini utu na utaifa wao tofauti na watanganyika.

‘’Roho ya uhanga kwa ajili  ya kabila, ukoo, jamii au taifa lake imeumbwa na Mungu  ndani ya kila mwanadamu na kuzuia utendaji wake ni dhambi . Hivyo Watanganyika nao lazima  Wafuate nyayo za Wazanzizar katika hilo,’’alieleza Mchungaji  Mtikila.


0 Responses to “ WAZANZIBAR ‘WAMKUNA’ MTIKILA.”

Post a Comment

More to Read