Tuesday, April 8, 2014

WAJUMBE WAKIMBILIA USAFIRI WA BODA BODA.




Baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba wameamua kutumia usafiri wa pikipiki katika  mizunguko yao mjini  Dodoma, ikiwa ni miongoni  mwa hatua za kupunguza  ghalama.

wajumbe kadhaa kutoka  kundi la 201 wakiwa katika  mizunguko  ndani ya mji wa Dodoma  kwa kutumia  usafiri wa pikipiki.
 Ghalama za teksi  kwa safari za katikati ya mji ni sh 3,000 wakati pikipiki ni sh 1,500 hadi sh 1,000 kulingana na mapatano kati ya abilia na mwendesha pikipiki.

Kutokana na uwamuzi huo, madereva teksi  wamekuwa wakilalamikia  kutoona tofauti ya mapato kwa siku kati ya Bunge la katiba na Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania. 

‘’Matumaini yetu  ni kufanya  Biashara kubwa wakati huu wa Bunge la katiba, lakini hali imekuwa sawa tu na Bunge la Jamuhuri ya muungano,’’ alisema dereva teksi, Said Yasin.

0 Responses to “ WAJUMBE WAKIMBILIA USAFIRI WA BODA BODA.”

Post a Comment

More to Read