Monday, April 7, 2014

RWANDA YAKUMBUKA MAUAJI YA KIMBARI.





Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi wenye msimamo mkali.

Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 , kipindi ambacho mauaji ya kimbare yalifanyika.

Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa inasema kuwa balozi wake ataiwakilisha nchi hiyo.

Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda, walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka 1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana
Alifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa katika anga ya Kigali na kudunguliwa.

Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.

Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994 wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.

Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita
Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria maombi kuwakumbuka maelfu waliouawa .

0 Responses to “RWANDA YAKUMBUKA MAUAJI YA KIMBARI.”

Post a Comment

More to Read