Sunday, June 22, 2014
ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII.
Do you like this story?
Serikali
imeombwa kulipa kipaumbele suala la umuhimu wa makundi ya walemavu kupewa haki
zao za msingi ikiwemo elimu kufuatia utafiti uliofanywa na wataalama wa
kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini kubaini kuwa asilimia
98% ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawaendi shule kwa sababu mbali mbali
ikiwemo dhana potofu iliyopo miongoni mwa jamii.
Akizungumza na mamia ya wananchi katika
kijiji cha Duga kilichopo kata ya Duga wilayani Mkinga katika zoezi la
kuhamisisha jamii kuwapatia haki zao za msingi walemavu mtaalam wa
kuhudumia walemavu kutoka nchini Thailand Dr,Kirsi Salo amesema katika
utafiti wao walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini baadhi yao wamefichwa
majumbani kutokana na imani haba za kishirikina kuwa kuzaa mtoto mlemavu
ni mikosi ndani ya familia na baadhi ya familia hudiriki hata kupoteza maisha
yao.
Kwa upande wake kiongozi wa kanisa la
kilutheri usharika wa Duga mchungaji Clementi Hongele ambaye amedai kuwa kati
ya walemavu 600 waliopo wilayani Mkinga kata ya Duga ndiyo inayoongoza kwa kuwa
na idadi kubwa ya walemavu na kusisitiza kuwa suala la unyanyapaa lililojengeka
miongoni mwa jamii hasa kwa jamii ya wafugaji imekuwa ndio chanzo cha kuwaficha
watoto wao walemavu katika vyumba maalum badala ya kuwapaleka katika shule
maalum ambazo zinawajengea uwezo wa kimaisha.
Mmoja kati ya wazazi wenye watoto
walemavu Bibi Mwanakombo Bakari analishukuru umoja wa makanisa kutoka nchini
Finland na mashirika ya kimataifa yanayoshirikiana na kanisa la kiinjili la
kilutheri (KKKT) dayaosos ya kaskazini mashariki kwa kusaidia walemavu wa kata
hiyo bila kujali itikadi za kidini hatua ambayo imesaidia kuondoa dhana potofu
ya unyanyapaa hasa baada ya wanavijiji kupewa elimu kuhusu athari na madhara ya
kuwaficha watoto wenye ulemavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII.”
Post a Comment