Wednesday, June 11, 2014

KESI YA WATANZANIA WATATU DHIDI YA KESI YA, RWANDA,UGANDA YAANZA KUNGURUMA



Kesi iliyofunguliwa na watanzania watatu ally hatibu Msangi, david  makatha na john bwenda katika mahakama  ya jumuiya ya afrika mashariki (EAC) wakiomba  itoe zuio la muda kwa Kenya ,Uganda,na Rwanda kufanya vikao bila kuzishrikisha tanzania na Burundi imeanza kunguruma.

Katika siku hiyo ya kwanza juzi hoja na malumbano ya kikanuni vilikwamisha  shauri hilo lonalosikilizwa  na jopo la majaji watano wakiongozwa  na jaji kiongozi jean bosco butasi baada ya wakili amable malala anayemwakilisha mwanasheria mkuu wa Rwanda  kuibua hoja ya kutopatiwa nyaraka za shauri  hilo kama kanuni za 14 na 15 za mahakama hiyo inavyoeleza.

Watanzania hao wanaowakilishwa na wakili jimmy obedi wa dar es salaam watajibu hoja za rwanda kabla ya juli 7 mwaka huu na baada ya hapo mahakama itapanga siku ya kusikiliza shauri  hilo linalovuta hisia za watu  wa Afrika mashariki  walalamikaji hao pia waliomba mahakama kuzizuia nchi hizo tatu  kutekeleza makubaliano  ya vikao vya enthebe Uganda Mombasa Kenya  na Kigali, Rwanda  bila kuzishirkisha  Tanzania na Burundi  hadi shauri litakaposikilizwa  na kuamuliwa.

Mdaiwa wa kwanza katika shauri ni katibu mkuu wa EAC anayewakilishwa na waakili dk antony kafumbe mwanasheria  mkuu wa Kenya  ambaye ni mdaiwa wa pili anawakilishwa na mawakili wawili Emanuel bita na pete ngumi.

Mdaiwa watatu ni mwanasheria mkuu wa Uganda anayewakilishwa na mawakili watatu Elisha bafirawala , Richard adrole na mureen ijang’ mwanasheria  wa Rwanda  ni mdaiwa wanne

0 Responses to “KESI YA WATANZANIA WATATU DHIDI YA KESI YA, RWANDA,UGANDA YAANZA KUNGURUMA”

Post a Comment

More to Read