Wednesday, June 11, 2014

MBUNGE ASEMA MALAWI IMEANZA KUWATISHA WATANZANIA



Mzozo kati ya Tanzania  na Malawi huenda ukaanza upya baada ya mbunge wa ileje  (CCM) aliko kibona kusema bungeni kwamba ndege za Malawi zimekuwa zikiruka katika anga ya Tanzania na kuwatisha wananchi.

Kwa kuzingatia uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Malawi naomba mwongozo wako  maana ndege za nchi hii sasa zinaingia hadi Tanzania na kuwatia hofu wananchi alisema kibona.

Kauli ya mbunge huyo imekuja wakati msimamo  rais wa Malawi profeser peter mutharika  kuhusu mzozo  uliopo kati  ya nchi hiyo na Tanzania kuhusu ziwa nyasa ukiwekwa bayana hatakuwa na mjadala kuhusu  mpaka wan chi hizo akidai kuwa ziwa nyasa ni la Malawi pekee.

Kibona amesema kwa takribani wiki mbili sasa ndege hizo zimekuwa zikionekana upande wa Tanzania  lakini hakuna kuli yoyote iliyotolewa  na serikali hadi sasa.

Katika mwongozo wake spika anne makinda amesema jambo hili ni umuhimu sana hivyo serikali ni lazima ijipange ili kulijibu aidha naibu spika job ndugai aliongeza hili jambo ni zito na serikali haiwezi kukurupuka  kujibu kwanza lazima majibu hayo yamfikie rais jakaya kikwete.

Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana ziwa Malawi ni mali ya Malawi  na litaendelea kuwa la Malawi daima aliwaambia wananchi hao huku akimshutumi mtangulizi wake joyce banda kwamba alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursa kwa Tanzania  kutumia udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.

Hata hivyo akizungumza bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard membe alisema Tanzania ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uchunguzi  wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya  kazi na serikali yoyote itkayoingilia madarakani

Juhudi za usuluhisho wa mzozo huo zinafanyika chini ya uongozi wa rais mstaafu wa msumbuji Joachim chisano akisaidiwa na rais mstaafu wa afrika kusini thabo Mbeki

0 Responses to “MBUNGE ASEMA MALAWI IMEANZA KUWATISHA WATANZANIA”

Post a Comment

More to Read