Saturday, June 14, 2014

TAARIFA KAMILI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU VISIWANI ZANZIBAR ,MTU MMOJA APOTEZA MAISHA,WENGI WAJERUHIWA



Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi la bomu kisiwani Zanzibar.
Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katika msikiti mmoja ulioko katika mji mkuu wa Stone Town.

Ni shambulizi la pili la bomu mwaka huu.Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo ambalo linajiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu katika kisiwa hicho.
Mnamo mwezi February, mabomu mawili tofauti ya kujitengezea yalilipuliwa nje ya kanisa Anglikana mjini Stone Town pamoja na mgahawa uliokuwa karibu na kanisa hilo.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.

via>>bbc

0 Responses to “TAARIFA KAMILI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU VISIWANI ZANZIBAR ,MTU MMOJA APOTEZA MAISHA,WENGI WAJERUHIWA”

Post a Comment

More to Read