Friday, June 13, 2014

UJUMBE HUU ALIOUTOA MONALISA KWA WALE WANAODAI HASTAHILI KUPOKEA POLE ZA GEORGE TYSON UNAUMIZA KWA KWELI



Muigizaji wa filamu nchini Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ambaye pia aliwahi kuwa mke wa marehemu George Tyson aliyefariki dunia kwa ajali ya gari wiki kadhaa zilizopita, amefunguka kupitia Instagram kuelezea kusikitishwa kwake na majungu ya watu kuwa hakustahili kupewa pole kufuatia msiba huo.

Monalisa ameandika: /Let me clear the air.ni hivi,pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George ktk maisha yetu,kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwengine..bt kwa macho ya kiMungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala.anayesema mke wa tyson alijifungia ndani mm nikawa nachukua pole zisizo zangu,dah!kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio mmoja.na wote walijifungia ndani,kwanini?ni wakristo na wanaijua dini.waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi,ni kwann?jiulize kabla ya kuropoka halafu ww ni mwanamke kuna siku yatakukuta.nilienda kutimiza wajibu wangu kama mke,ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana,nimekaa msibani naambiwa nachukuwa pole za bure.wacha nikukumbushe maandiko 'Alichokiunganisha Mungu?.;kilichofungwa duniani?"¦..;nikupende,nikutunze hadi kifo?¦.. sasa kifo kimetutenganisha.siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani?pamoja na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu esp.miaka 5 ya mwisho wa uhai wake.acheni nimlilie he was my best friend 1998-2014.nimeshare nae kitanda 2000-2006.nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu?ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu..na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini,mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe,na akifa?and for ur info..msianze anajifanya mke ss hv ili apewe mali..Sonia ni mali kubwa sana alioniachia am so happy.waaache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie.mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki?niacheni nimlilie,waacheni fans wangu walie na mm.

George Tyson anatarajiwa kuzikwa Jumamosi ya June 15 kwao Kisumu Kenya.

0 Responses to “ UJUMBE HUU ALIOUTOA MONALISA KWA WALE WANAODAI HASTAHILI KUPOKEA POLE ZA GEORGE TYSON UNAUMIZA KWA KWELI ”

Post a Comment

More to Read