Thursday, June 19, 2014

VODACOM YAWAANGUKIA WATEJA WA M- PESA



Kampuni ya simu za mkononiya Vodacom imewaomba radhi wateja wake wanatumia  huduma ya mpesa kutokana  na hitilafu  za kiufundi zilizosababisha  kusimama kwa huduma hiyo kwa siku kadhaa.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, rene meza alisema dare s salaam jana :  ninawaomba radhi wateja  wetu ambao  wamekuwa na wakati mgumu kupata huduma ya  M PESA   katika siku chache zilizopit. Tunatambua umuhimu  wa huduma hii kwa  hali iliyoyojitokeza ilikuwa nje ya uwezo wetu na kamwe hatutaitarajia .

Meza alisema kilichotokea kwenye mfumo wa M pesa  ni changamoto ambayo mfumo wowote unaotumia teknolojia inaweza kukumbana  nayo bila kutarajia lakini jambo la muhimi ni kwa jinsi gani mtoa huduma nabyoweza kujipanga kiutatua kwa haraka kudhibiti  madhara makubwa zaidi  kwa wateja .

Kuhusu usalama wa fedha  meza aliwahakikishia wateja wa Vodacom na wabia wanaotumia huduma hiyo kwamba fedha  zote zipo salama na zinalindwa kwani kilichotkea ni wateja  kushindwa kupta huduma hiyo kwenye simu zao za mkononi  na siyo tatizo kwenye mfumo mzima wa M PESA.

Hakuna madhara ya kibiashara kwetu ila kutokana na M pesa  kuta tegemeo kwa mamilioni ya watanzania ktika maisha yao ya kila siku ikiwa ndio huduma kinara ya fedha kwa njia ya simu za mkonini ni wazi kwamba imeleta sumbufu mkubwa kwa watumaji.

0 Responses to “VODACOM YAWAANGUKIA WATEJA WA M- PESA”

Post a Comment

More to Read