Monday, July 21, 2014

KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YAZINDULIWA RASMI MKOA WA NJOMBE.


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akiwa Ametoka Kupima VVU Mara Baada ya Kuzindua Kampeni ya Upimaji wa Hiari Huko Lupembe Barazani-MAJIBU SIRI Yake.

Wakazi wa Lupembe wakishuhudia Uzinduzi wa Kampeni ya Upimaji Mkoa wa Njombe Lupembe Barazani.


Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu Aseria Msangi Jana Amezindua Kampeni ya Upimaji wa Virusi Vya Ukimwi Kwa Hiari Kwa Vijana Ikiwa ni Mpango Mkakati wa  Mkoa wa Njombe Kwa Kushirikiana na Wadau Mbalimbali Katika Kuhakiki Mambukizi ya Mapya ya Virusi Vya Ukimwi Yanashuka Katika Kipindi cha Miaka Mitano.

Akizungumza Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Kwenye Uzinduzi wa Kampeni Hiyo Iliyofanyika Kimkoa Katika Kijiji cha Lupembe Barzani Wilayani Njombe , Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Amesema Kutokana na Vifo Vinavyosababishwa na Ugonjwa wa Ukimwi Vimechangia Kuwepo Kwa Idadi Kubwa ya Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Magumu na Mitaani.

Ameongeza Kuwa Vifo Hivyo Pia Vimechangia Watoto Wengi Kujiingiza Katika Ajira Zisizo Rasmi , Vitendo Vya Uhalifu Pamoja na Mateso na Wale Wanaolelewa na Ndugu Wakati Mwingine Wanakosa Haki za Msingi Ikiwemo Elimu.

Kwa Upande Wake  Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Njombe Abubakary Magege Amesema Kuwa  Kiwango cha Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Mkoani Hapa Bado Ipo Juu , Hivyo Jamii Inapaswa Kujitokeza Kwa Wingi Kupima Afya Zao  Ili Kudhibiti  Maambukizi Mapya Virusi Vya Ukimwi.

Wakizungumza Mara Baada ya Kupima Afya Zao Baadhi ya Wakazi wa Vijiji Vya Tarafa ya Lupembe Wamesema Kuwa Kutokana na Uhamasishaji Mkubwa Unaofanywa na Serikali Wameona ni Vyema Wakaiunga Mkono Jitihada Hizo Kwa Kujitokeza Kupima Ili Wafahamu Afya Zao na Kuhakikisha Nguvu Kazi ya Taifa Haipotei,

0 Responses to “KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YAZINDULIWA RASMI MKOA WA NJOMBE.”

Post a Comment

More to Read