Sunday, September 7, 2014

07 Sep 2014 WAFANYABIASHARA WADOGO WANAOUZA PEMBEZONI MWA BARABARA KUU MJINI NJOMBE WATAKIWA KUHAMIA ENEO JINGINE.


Akizungumza na Wafanyabiashara Hao Baada ya Kupokea Maelekezo ya Kisheria Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo,Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Agrey Mtambo




Sakata la Wafanyabiashara Wadogowadogo Wanaofanya Biashara Zao Pembezoni Mwa Barabara Kuu Mjini Njombe Limeendelea Kutikisa Katika Mji wa Njombe Kufuatia Wafanyabiashara Hao Kuandamana Hadi Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Leo Kufuatia Oparesheni ya Kuwaondoa Inayoendelea.

Wafanyabiashara Hao Wamelazimika Kwenda Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Baada ya Viongozi Ngazi ya Mtaa na Kata ya Njombe Mjini Kuendesha Oparesheni ya Kuwahamisha Katika Maeneo Hayo Kwa Madai Sio Maeneo Sahihi Kwa Biashara Kwa Mujibu wa Sheria ya Barabara.

Akizungumza na Wafanyabiashara Hao Baada ya Kupokea Maelekezo ya Kisheria Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo,Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Agrey Mtambo

Amesema Kuwa Licha ya Mazungumzo ya Muda Mrefu Baina Yake na Serikali Lakini Bado Mwafaka Haujapatikana Ambapo Majibu Zaidi Yatatolewa Wiki Lijalo Siku ya Juma Nne.

Bwana Mtambo Amesema Kuwa Katika Mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Wamekubaliana Wafanyabiashara Hao Kwa Sasa Wafanyie Katika Eneo Lolote Ndani ya Mji wa Njombe Isipokuwa Kwenye Barabara Kuu ya Njombe Songea.

 
Pamoja na Kukubaliana Kwa Maagizo Hayo ya Kufanyabiashara Kwenye Maeneo Tofauti na Barabara Kuu Lakini Bado Wafanyabiashara Hao Wameonekana Kuendelea Kuitupia Lawama Serikali Kwa Kuwanyanyasa Katika Biashara Zao.

Wamesema Awali Walifukuzwa Katika Eneo Hilo na Kuambiwa Warudi Nyuma Lakini Bado Tena Wanaendelea Kufukuzwa na Kuharibiwa Mali Zao.

 
Kwa Upande Wake Ispekta Martinus Mirumbe Amewataka Wafanyabiashara Hao Kuzingatia Maagizo Yanayotolewa na Viongozi Wao Ikiwa ni Pamoja na Kutii Amri Bila Shuruti.
Na Gabriel Kilamlya

0 Responses to “ 07 Sep 2014 WAFANYABIASHARA WADOGO WANAOUZA PEMBEZONI MWA BARABARA KUU MJINI NJOMBE WATAKIWA KUHAMIA ENEO JINGINE.”

Post a Comment

More to Read