Sunday, September 7, 2014

STARS 'MACHO KWA MACHO' NA BURUNDI, KULIPA KISASI CHA KUPIGWA 3-0?




TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo inachuana na Burundi mjini Bujumbura katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopo katika kalenda ya FIFA.

Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-0 na Burundi katika mechi maalumu ya kirafiki kuadhimisha miaka 50 ya Muungano, Aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Hata hivyo kikosi kilichocheza katika mechi hiyo kilisheheni wachezaji waliotokea katika mpango maalumu wa TFF wa maboresho ya Taifa Stars ambapo wachezaji wengi hawapo isipokuwa Joram Mgeveke wa Simba.
Nahodha wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema timu imeandaliwa vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.

Kuhusu wachezaji wawili hatari wa Burundi wanaokipiga ligi kuu Tanzania bara, Amiss Tambwe (Simba) na Didier Kavumbagu (Azam fc) Cannavaro alisema ni wachezaji wa kawaida na wameshawazoea, hivyo hawawezi kuwapa shida.

“Ni wachezaji wa kawaida tu, tunakutana nao kila siku, nadhani tutapambana vizuri na tutapata ushindi”. Alisema Cannavaro.
“Hata sisi tunawafahamu Amiss (Tambwe) na Didier (Kavumbagu).
“Tunawafahamu udhaifu wao na wao wanatufahamu, hata mimi naweza kufunga kutokana na ujuzi wangu”.

“Hata tulipokwenda Msumbiji tulicheza vizuri na tulipata goli, lakini hatakufanikiwa kusonga”. Alisema Cannavaro.

Kila la heri Taifa stars katika mchezo wa leo.

0 Responses to “STARS 'MACHO KWA MACHO' NA BURUNDI, KULIPA KISASI CHA KUPIGWA 3-0?”

Post a Comment

More to Read