Tuesday, September 9, 2014
JAJI RAMADHAN RAISI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU.
Do you like this story?
Mahmoud Ahmad Arusha
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu imemteua Jaji mkuu mstaafu wa
Tanzania Agustino Ramadhan kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka miwili
uteuzi huounaanza mara moja baada ya aliyekuwa rais wa mahakama hiyo Sophia
Akuffo wa Ghana kumaliza muda wake.
Jaji Ramadhani Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti hicho tangia
kuanzishwa kwa mahakama hiyo baada ya kupata kura 7 kwa kura nne dhidi ya
mpinzania wake katika nafasi hiyo ya rais wa mahakama hiyo huku nafasi ya
makamu wake ikichukuliwa na jaji Eisie Thompson kutoka nchi ya Nigeria.
Katika nafasi hiyo ya makamu walikuwepo majaji watatu waliokuwa wakiwania
nafasi hiyo na baada ya upigaji wa kura mara ya kwanza wawili walifungana kwa
kura 4 na mmoja kupata kura tatu ndipo uchaguzi ulirudiwa na jaji Thompson
kuibuka mshindi kwa kupata kura 6 dhidi ya tano za mpinzani wake.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi huo jaji Ramadhan
alisema kuwa ni heshima kwa Taifa la Tanzania kwani ndio mara yake ya kwanza
kupata nafasi hiyo huku akisema kuwa nafasi hiyo ni heshima kwake na kwa taifa
lake.
“Kesi yeyote inayohusu nchi yangu mimi sitakuwepo kutokana na sheria zetu
za mahakama hii na kuwa tayari watanzania watano wamefungua kesi kwenye
mahakama hii na kesi mbili zimetolewa hukumu ya mchungaji mtikila na
Zongo”alisema jaji Ramadhan
Alisema kuwa mpaka sasa ni kesi 5 zimefunguliwa katika mahakama
hiyo na mbili teyari zimetolewa ikiwemo dhidi ya serekali ya Tanzania kesi
iliyofunguliwa na mchungaji Christopher Mtikila iliyohusu mgombea Binafsi huku
akisema kuwa kuchukuwa hatua kwa utekelezaji wa hukumu kunategemea na serekali
kama imejiunga na mikataba ya kimataifa.
Alitanabaisha kutokana na sheria za mahakama hiyo wakati wa usikilizaji
wa kesi zinazoihusu nchi yetu yeye hawezi kuisikiliza na kuwa Atajitoa
kuisikiliza kama shiria ilivyo ya mahakama hiyo huku akisema mahakama hiyo
inaundwa na majaji 11 kutoka nchi tofauti za bara hili .
Aidha mahakama hiyo iliwaapisha majaji watatu wa mahakama hiyo kabla ya
kuanza mchakato wa upigaji kura kumteuwa jaji wa mahakama hiyo huku ripoti ya
mahakama hiyo kila mwaka ikipelekwa kwa umoja wan chi za Afrika.
Uchaguzi huo huwa ni vipindi vya miaka miwili miwili na iwapo ukimaliza
muhula wa kwanza kama utateuliwa tena kushika nafasi hiyo utakuwa ndio kipindi
chako ya mwisho kushikilia nafasi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JAJI RAMADHAN RAISI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU.”
Post a Comment