Sunday, October 12, 2014
ABIRIA ALIYEFIA UWANJA WA NDEGE AZUA TAHARUKI, KIFO CHAKE CHAHUSISHWA NA EBOLA
Do you like this story?
TAHARUKI imezuka
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi nchini
Kenya, leo asubuhi baada ya abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki dunia muda mfupi
alipowasili uwanjani hapo.
Abiria huyo mwanamke
alikuwa akitokea Juba, Sudan Kusini lakini kukawepo tetesi kuwa huenda
amefariki kwa ugonjwa wa Ebola.
Vipimo vya madaktari
vimeonesha kuwa mgonjwa huyo hakufa kwa Homa ya Ebola. Katibu wa Afya wa
Baraza la Mawaziri nchini Kenya, James Macharia amethibitisha kuwa mgonjwa huyo
hakuwa na Homa ya Ebola.
Mashuhuda wa tukio
hilo wamesema kuwa waliwaona maofisa wa afya wakielekea katika Kliniki ya Port
ambapo mgonjwa huyo alikimbizwa kabla ya mauti kumfika.
Viwanja vya ndege ni
baadhi ya maeneo yaliyo katika uangalizi kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola
ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya 4,000 kwenye ukanda wa magharibi mwa
Afrika.
Shirika la Ndege la Kenya Airways lilisitisha safari zake katika ukanda wa magharibi mwa Afrika kwa kuogopa maambukizi ya ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ABIRIA ALIYEFIA UWANJA WA NDEGE AZUA TAHARUKI, KIFO CHAKE CHAHUSISHWA NA EBOLA ”
Post a Comment