Thursday, October 9, 2014
MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA.
Do you like this story?
Na.
Aron Msigwa-MAELEZO.
Mfumuko
wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 6.6
kutoka asilimia 6.7 iliyokuwepo mwezi Agosti kutokana na kupungua kwa bei ya
bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu
za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa
za vyakula zikiwemo mchele, mahindi, ulezi, matunda, Sukari na
vinywaji baridi zimechangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini
Bidhaa
nyingine zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini ni Sare za shule,
Simu za mkononi, runinga na viatu huku akibainisha kuwa Fahirisi za bei kwa
maana ya kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma
zinazotumiwa na kaya nchini zimeongeka na kufikia 149.93 kwa mwezi
Septemba 2014 ikilinganishwa na 140.61 za mwezi Septemba mwaka jana.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.4 kwa mwezi Septemba 2014 ikilinganishwa na asilimia 0.1 za mwezi Agosti kutokana na kuongezeka kwa Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo samaki, matunda, mbogamboga, mihogo na vinywaji baridi, mkaa, mazulia na dawa za Binadamu kuwa na mchango mkubwa katika ongezeko la fahirisi.
Aidha,
amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua
hadi asilimia 8.3 mwezi Septemba 2014 kutoka asilimia 8.5 za mwezi Agosti 2014
na kuongeza kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma za jamii kwa mwezi Septemba, 2014 umefikia shilingi 66
na senti 70.
Kwa
upande wa mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Bw.
Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana, Kenya ukipungua na kufikia
asilimia 6.6 kwa mwezi Septemba kutoka 8.34 za mwezi Agosti huku Uganda ikiwa
na mfumuko wa bei wa asilimia 1.4 mwezi Septemba kutoka asilimia 2.8 za mwezi
Agosti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA. ”
Post a Comment