Wednesday, October 8, 2014
SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LATOA PONGEZI KWA BUNGE MAALUM LA KATIBA KWA KAZI NZURI.
Do you like this story?
SHIRIKISHO la Muziki Tanzania limetoa pongezi za dhati kwa Bunge
Maalum la Katiba lililokuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe.
Samuel Sitta kwa kuingiza Ibara tatu katika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
huko mjini Dodoma.
Pongezi hizo zilitolewa jana na Rais wa Shirikisho hilo Bw. Addo November
alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari hapo jana huku akisema kuwa Rasimu
Inayopendekezwa imezingatia haki za Wasanii kwa kuingiza Ibara tatu zikiwemo Ibara
ya 15, ya 38 (II) na Ibara ya 56, 3 (e) ambazo Ibara hizo zinalinda kazi
za muziki na sanaa zote kwa ujumla.
Bw. November alieleza kuwa Shirikisho limefurahi kuona kuwa Sheria ya
inayohusu masuala ya kazi za sanaa katika nchini imeanza kutekelezwa Kikatiba
kama ilivyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, Rwanda na Uingereza.
“Kwa kubainisha ibara hizi katika Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa,
zinaonyesha ulindaji wa Hati Miliki(Intellectual
property) za Wasanii na kazi zao na hii itasaidia kuboresha maisha ya
wasanii kimapato kwa kupitia kazi zao kwani Katiba hii itawalinda
wasanii Kisheria”, alisema November.
Aliongeza kuwa Shirikisho limeingia Mkataba na Kampuni ya JB Belmont kwa
kuweza kuwapatia wasanii na waandishi wa habari punguzo la bei katika huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Aidha, November aliwashauri waandishi wa habari kuunda Shirikisho la
Waandishi wa habari la muziki kwani hii itasaidia kupata na kutoa taarifa
mbalimbali kwa jamii zinazohusu masuala ya muziki kwa kuaangalia walikotoka na
wanakoelekea kimaendeleo.
Naye Meneja Mahusiano wa Kampuni ya JB Belmont, Bi. Gillian Macheche
alisema kuwa kutakuwa na punguzo la asilimia 40 kwa huduma mbalimbali ikiwemo
kukodi Ukumbi wa Mkutano, Vyumba vya kulala wageni, vyakula na Vinywaji kwa
wasanii na waandishi wa habari.
Kwa upande mwingine Mjumbe wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwanamuziki
mkongwe nchini Bw. Kassim Mapili alitoa shukrani zake za dhati kwa
waandishi wa habari kwa kutoa taarifa kwa umma juu ya afya yake
pamoja na jamii kwa ujumla kwa kumsaidia katika kipindi chote alichokuwa
akitibiwa ugonjwa wa Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LATOA PONGEZI KWA BUNGE MAALUM LA KATIBA KWA KAZI NZURI.”
Post a Comment