Monday, November 17, 2014
KOCHA JUMA MWAMBUSI WA MBEYA CITY AJIUZULU
Do you like this story?
Ripoti kadhaa ambazo
hazijathibitishwa na uongozi wa mbeya city zinasema kuwa kocha wa timu hiyo
Juma Mwambusi amejiuzulu .
Hatua hiyo imekuja
baada ya kuishuhudia timu yake ikipata mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi
ambapo katika michezo saba imeweza kushinda mchezo mmoja pekee huku ikitoka
sare kwenye michezo miwili na kufungwa jumla ya michezo minne .
Taarifa mbalimbali
toka jijini Mbeya zinasema kuwa kwa muda mrefu wachezaji wa Mbeya City walikuwa
wamepoteza Imani na kocha wao hali ambayo mashabiki wanaamini kuwa imechangiwa
na pengo la aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalusi .
Mwalusi ambaye
alihama Mbeya City na kwenda kuifundisha timu ya ligi daraja la kwanza ya
Panoni Fc ya mjini Moshi anadaiwa kutoridhishwa na kitendo cha kupewa ‘mgao
kiduchu’ wa zawadi ya kocha bora ambaye bosi wake Mwambusi aliipata hali ambayo
ilionyesha kutothaminiwa kwa mchango wake .
Hali ya Juma Mwambusi
ilikuwa inaonekana kuwa mbaya kadri Mbeya City ilivyozidi kupata matokeo mabaya
hasa baada ya kujikuta ikipoteza michezo minne mfululizo mbele ya timu za Azam
Fc , Mtibwa Sugar , Mgambo Jkt na Stand United.
Endapo taarifa hii
itathibitika kuwa Kweli Mwambusi ambaye msimu uliopita alitwaa tuzo ya kocha
bora wa msimu kabla ya kutwaa tuzo nyingine ya kocha bora wa mwezi septemba
wakati ligi ilipoanza atakuwa kocha wa pili kupoteza kibarua chake baada ya
Denis Kitambi ambaye alifukuzwa kazi na Ndanda Fc baada ya matokeo mabaya .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOCHA JUMA MWAMBUSI WA MBEYA CITY AJIUZULU ”
Post a Comment