Monday, November 17, 2014
TWAKIMU ZA LIGI KUU KUFIKIA RAUNDI YA SABA!
Do you like this story?
Baada ya kukamilika kwa raundi ya saba,
Mtibwa Sugar wapo kileleni kwa pointi 15 wakifuatiwa na Yanga katika nafasi ya
pili wakijikusanyia pointi 13.
Mabingwa watetezi Azam fc wapo nafasi
ya tatu wakijikusanyia pointi 13 sawa na Yanga, lakini wanazidiwa wastani wa
mabao ya kufunga na kufungwa.
Timu ya Ndanda fc inaongozwa kwa
kufungwa mabao mengi kwani mpaka sasa nyavu zake zimetikishwa mara 12.
Vinara Mtibwa Sugar ndio timu pekee
iliyofungwa magoli machache ambapo nyavu zake zimetikishwa mara tatu.
Timu zinazofuatia kufungwa mabao
machache ni Azam fc na Kagera Sugar ambazo zimefungwa mabao manne.
Timu ya Mtibwa Sugar inaongoza kwa
kufunga mabao mengi ambapo imetia kambani magoli 10, ikifuatiwa na Yanga,
Coastal Union zilizofunga mabao tisa.
Simba ni timu pekee inayoongoza kutoka
sare ambapo imetoka sare mara sita mfululizo.
Lakini Mnyama na Mtibwa Sugar ndio timu
pekee ambazo hazijafungwa mpaka sasa.
Timu za Mgambo JKT, Mbeya City fc na
Ruvu Shooting zinaongoza kwa kupoteza mechi nyingi ambapo zimefungwa katika
michezo minne. Ligi kuu Tanzania bara itaanza kutimua vumbi tena Desemba 26
mwaka huu na ratiba nzima iko hivi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TWAKIMU ZA LIGI KUU KUFIKIA RAUNDI YA SABA!”
Post a Comment