Wednesday, December 17, 2014
AKAMATWA KWA KUGHUSHI BIMA YA AFYA
Do you like this story?
Mtu mmoja aliyejifanya kuwa ni mfanyakazi wa Taasisi ya IMTU, Bakari
Ramadhani amekamatwa na maofisa wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF),
akiwa na fomu zao za kughushi za kuchukulia dawa zikiwa zimegongwa mihuri
inayoonyesha ni ya Hospitali ya Rufaa ya Temeke.
Ramadhani ambaye ni mkazi wa Kinondoni Mosco, alikamatwa jana ndani ya
duka la J.D anakodaiwa kwenda mara kwa mara kuchukua dawa. Inadaiwa mtu huyo
pia ameshafanya hivyo mara kadhaa mpaka kwenye matawi ya duka hilo. Aliwekewa
mtego na maofisa wa NHIF kwa kushirikiana na wafanyakazi wa duka hilo na
wakafanikiwa kumkamata.
Ramadhani ameiambia Fahari News kuwa anachukua dawa hizo kwa ajili ya
kuwasaidia ndugu zake 15 ambao ni wagonjwa.
Alisema amekwisha chukua dawa kwa mtindo huo katika matawi ya duka la J.D
ya Mlimani City, Kariakoo na Posta. Aliyataja maduka mengine kuwa ni Nakiete
Mwenge na Okinawa lililoko Temeke.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ AKAMATWA KWA KUGHUSHI BIMA YA AFYA ”
Post a Comment