Monday, December 8, 2014

BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA SUNDERLAND (SAFC) ZATANGAZA UTALII WA TANZANIA NA UINGEREZA


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya mpira ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo kutoka kulia ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bw. Geofrey Meena, Teddy Mapunda mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya (TTB) na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nestor Mapunda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi na kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Teddy Mapunda

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya ligi kuu ya Uongereza ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo huko Sunderland.



Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”

0 Responses to “BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA SUNDERLAND (SAFC) ZATANGAZA UTALII WA TANZANIA NA UINGEREZA”

Post a Comment

More to Read